Loading...

Wenger ameuomba uongozi wa Arsenal umwongeze miaka miwili

Kocha Arsene Wenger ameauambia uongozi wa Arsenal kwamba anataka kuendelea kubaki Emirates kwa miaka miwili.

Katika mkutano wa pamoja na uongozi wiki iliyopita, Wenger ameweka wazi yake ya moyoni kuwa angependa kubaki kwa miaka miwili zaidi ili afanye mabadiliko.

Kwa mujibu vya vyanzo vya habari, ni kwamba Wenger ameona makosa yalipo na anataka kubadilisha ndiyo maana anaomba miaka hiyo miwili ingawa haijaelezwa kuwa baada ya hapo ataondoka au ataendelea kubaki.

Hata hivyo, Wenger anaweza kuwa na wakati mzuri wa kupata mkataba mpya kama Arsenal itaitwanga Man City wikiendi hii.

Kama atafungwa atakuwa ameingia kwenye hofu mpya na huenda uongozi wa Arsenal unaweza kuamua tofauti.
Wenger ameuomba uongozi wa Arsenal umwongeze miaka miwili Wenger ameuomba uongozi wa Arsenal umwongeze miaka miwili Reviewed by Zero Degree on 3/30/2017 12:09:00 PM Rating: 5

Powered by Blogger.