Loading...

Wenye ulemavu wa ngozi [ualibino] mkoani Kigoma wadai kuchoshwa na maisha ya kambini

IDADI kubwa ya walemavu wa ngozi wanaoishi katika kambi ya Kabanga mkoani Kigoma, wamelalamikia ugumu wa maisha kambini hapo wakieleza kuwa wanatamani kurudi nyumbani.

Kituo cha Kabanga chenye walemavu mchanganyiko 246, kilianzishwa mwaka 2008 baada ya kuzuka mauaji ya watu wenye ulemavu wa ngozi. 

Wakizungumza katika mahojiano na Nipashe kambini humo, baadhi ya wenye ualbino walisema tangu waingie humo maisha yao yamekuwa magumu kupindukia.

Mmoja wao, Elizabeth Luchoma (28), alisema kitendo cha kuwazuia hata kwenda kusali kanisani kila Jumapili kwa hofu ya usalama wao ni sawa na kufungwa gerezani.

"Tangu nije hapa ni mwaka mmoja nilitokea kijiji cha Maji ya Moto kilochopo Katavi baada ya kukatwa mkono wa kulia na wauawaji. Lakini kuanzia wakati huo sina natamani bora nirudi nyumbani," alisema Luchome.

Aliongeza kuwa ana mume mwenye ualbino na watoto wanne ambao hawakuathirika ngozi.

Lucia Jonas (25) wa kijiji cha Kizenga Kigoma alisema anatamani kurudi nyumbani lakini viongozi wa kituo wanamkatalia.

Aliongeza kuwa tangu achukuliwe kwa gari la serikali kutoka kijijini kwake mwaka mmoja na nusu uliopita anaona kila kitu katika maisha yake kimesimama.

"Pamoja na ualbino wangu huu lakini nikiwa nyumbani nilikuwa nafanyabiashara ya magadi, hapa mambo ni magumu sana," alisema.

Mkuu wa kambi hiyo, Jocob Kitunga, alisema serikali hazuii watu kuondoka lakini hadi ijiridhishe na usalama wao.

"Kwa mfano, katika kipindi cha Januari na Machi mtu mmoja ameruhusiwa kuondoka baada ya mtoto wake kufikisha miaka minne," alisema.

Source: Nipashe
Wenye ulemavu wa ngozi [ualibino] mkoani Kigoma wadai kuchoshwa na maisha ya kambini Wenye ulemavu wa ngozi [ualibino] mkoani Kigoma wadai kuchoshwa na maisha ya kambini Reviewed by Zero Degree on 3/05/2017 11:13:00 PM Rating: 5

Powered by Blogger.