Baada ya 'Wapo' Nay adai usalama wake ni mdogo, ....atishiwa kifo na watu wasiojulikana
RAPA Nay wa Mitego ameeleza masikitiko yake huku akidai kuwa kuna watu wamekuwa wakimtumia ujumbe kwa njia ya simu wakimtishia usalama wa maisha yake kutokana na Wimbo aliouachia hivi karibuni wa WAPO akiwazungumzia viongozi wanaofoji vyeti na kujipatia ajira.
Nay ambaye aliachia WAPO ambao ulichukuliwa kama unawakashfu viongozi licha ya Rais John Magufuli na Waziri wa Habari, Utamaduni, Sanaa na Michezo, Dkt. Harrison Mwakyembe kuruhusu wimbo huo upigwe.
Nay anasema wimbo huo umesababisha baadhi wa watu wamchukie na wamekuwa wakimuwinda kila anapokwenda na kumtumiwa ujumbe wa vitisho jambo linalompa wakati mgumu na kujihisi muda wowote anaweza kufanyiwa kitu chochote.
“Namshukuru Rais Magufuli na Waziri Mwakyembe kwa kuruhusu WAPO ipigwe, wapo watu wengine hawajapenda, wamechukizwa na wimbo huo.
” Tangu WAPO itoke kuna watu hawataki kusikia ukweli, napigiwa simu nyingi kutishiwa, natumiwa meseji nyingi na watu kila mmoja anaongea la kwake, imefika wakati naishi kama ndege kwani nawindwa.
“Naweza kuwa natoka sehemu naenda nyumbani, nafuatwa kuonyesha naelekea wapi…. Imefika wakati hata familia yangu sasa naanza kuionea huruma…..” Amesema Nay.

Source: GlobalPublishers
Baada ya 'Wapo' Nay adai usalama wake ni mdogo, ....atishiwa kifo na watu wasiojulikana
Reviewed by Zero Degree
on
4/04/2017 11:56:00 PM
Rating: