Loading...

Bayern Munich yaingia katika vita kubwa dhidi ya Klabu ya Chelsea

Bayern Munich wanataka kuitibulia Chelsea katika mbio za kumuwania winga mahiri wa Bayer Leverkusen, Julian Brandt na inadaiwa kuwa wapo tayari kutoa dau la Euro 30 milioni kwa ajili ya staa huyo mwenye umri wa miaka 20.

Brandt anaweza kuwa mbadala wa winga wa kimataifa wa Brazil, Douglas Costa ambaye kuna uwezekano mkubwa akaondoka Allianz Arena mwishoni mwa msimu huu baada ya kukosa namba ya kudumu kikosini.

Wakati huohuo, Manchester City imeingia katika mbio za kumnasa mlinzi mahiri wa Burnley na timu ya taifa ya England, Michael Keane, licha ya kuelezwa kwamba Everton ipo katika nafasi nzuri zaidi ya kumtwaa staa huyo.,

Keane aliyeachwa na Manchester United miaka mitatu iliyopita ameibuka kuwa mmoja kati ya walinzi bora wa kati Ligi Kuu ya England kiasi cha kuitwa katika kikosi cha timu ya taifa ya England na amekuwa akisakwa na timu kubwa.
Bayern Munich yaingia katika vita kubwa dhidi ya Klabu ya Chelsea Bayern Munich yaingia katika vita kubwa dhidi ya Klabu ya Chelsea Reviewed by Zero Degree on 4/04/2017 11:58:00 PM Rating: 5

Powered by Blogger.