Loading...

Biashara ya Pembe za Faru yaruhusiwa Afrika Kusini

Wakati Tanzania pamoja na nchi za Afrika Mashariki zikipambana na biashara ya pembe za faru, Mahakama ya katiba ya Afrika kusini imelipinga jaribio la serikali la kutaka kuweka marufuku kwa biashara ya pembe za faru katika matumizi ya ndani.

Matokeo yake ni kwamba pembe hizo za faru zinaweza kuuzwa ndani ya nchi huku marufuku katika biashara hiyo kimataifa ikiwa bado inaendelea.

Watunzaji wa wanyama pori hao wamedai kuwa, kuruhusu biashara hiyo kuendelea kufanyika kihalali kutaweza kupunguza idadi ya faru wanaouwawa kutokana na kwamba pembe za faru zinaweza kukatwa na kuacha wanyama hao hai.

Hata hivyo wahifadhi wa wanyama pori hawakubaliani na hatua hiyo.
Biashara ya Pembe za Faru yaruhusiwa Afrika Kusini Biashara ya Pembe za Faru yaruhusiwa Afrika Kusini Reviewed by Zero Degree on 4/06/2017 08:24:00 PM Rating: 5

Powered by Blogger.