Loading...

Mpya kuhusu sakata la Roma Mkatoliki kukamatwa

Habari za kukamatwa mwanamuziki ROMA Mkatoliki zinaendelea kuchukua sura mpya tangu alipochukuliwa na watu wasiojulikana akiwa katika studio za Tongwe zilizopo Masaki, Dar es Salaam.

Kituo cha Runinga cha Azam TV kimefanya mazungumzo na Kamanda wa Polisi Mkoa wa Kipolisi Kinondoni, Suzan Kaganda kuhusu kukamatwa kwa ROMA kama kuna taarifa zozote kutoka kwenye jeshi hilo.

RPC Kaganda amewambia kuwa kwa sasa bado hawana taarifa yoyote na hivyo kuwataka wananchi kutulia wakati wao wakiendelea na uchunguzi na baada ya masaa 48 watatoa taarifa kuhusu hatua waliyofikia.

Taarifa hiyo inakuja wakati mke wa ROMA, Nancy akiendelea kuomba vyombo vya usalama na Watanzania kwa ujumla kuungana kumtafuta mumewe ambaye amedai kuwa bado anamuhitaji na hata familia inamtegemea.
Mpya kuhusu sakata la Roma Mkatoliki kukamatwa Mpya kuhusu sakata la Roma Mkatoliki kukamatwa Reviewed by Zero Degree on 4/06/2017 11:09:00 PM Rating: 5

Powered by Blogger.