Loading...

Vyama vya siasa nchini Kenya vyaruhusiwa kujihesabia kura kwenye uchaguzi mkuu

Maofisa wa tume huru ya uchaguzi nchini Kenya, IEBC, wakiwa katika shughuli ya kuandikisha wapiga kura wapya (Picha ya mtandao)
Tume ya uchaguzi nchini Kenya imekubali kuruhusu vyama vya kisiasa kujihesabia kura kwenye uchaguzi mkuu ambao utafanyika tarehe 8 mwezi Agosti mwaka huu.

Hata hivyo tume hiyo ilisema kuwa ndiyo ina ruhusa ya kutangaza matokeo ya mwisho.

Kiongozi wa upinzani Raila Odinga alizua wasi wasi mwishoni mwa wiki baada ya kuwaambia wafuasi wake kuwa muungano wa upinzani wa Nasa, utabuni kituo chake cha kuhesabu kura na kutangaza matokeo ya uchaguzi huo.

Viongozi wa upinzani wanasema kuwa kuwepo kituo hicho itasaidia kuzuia udanganyifu kwenye uchaguzi.

Rais Uhuru Kenyatta anawania uchaguzi kwenye muhula wa pili na anatarajia kuukabili mungano wa vyama vikuu vya upinzani.
Vyama vya siasa nchini Kenya vyaruhusiwa kujihesabia kura kwenye uchaguzi mkuu Vyama vya siasa nchini Kenya vyaruhusiwa kujihesabia kura kwenye uchaguzi mkuu Reviewed by Zero Degree on 4/06/2017 11:20:00 PM Rating: 5

Powered by Blogger.