Loading...

Bosi RwandaAir atimuliwa kazi

Shirika la Ndegee la Rwanda, RwandAir limemtimu kazi Afisa Mtendaji Mkuu wa shirika hilo, John Mirenge na nafasi yake kuchukuliwa na Chance Ndagano.

Uamuzi wa kuachishwa kazi umetolewa na kamati maalum iliyoundwa na Rais wa Rwanda, Paul Kagame kuchunguza utendaji kazi wa Mirenge huku sababu ya kuachishwa kazi ikiwa haijawekwa wazi.

Mirenge ametimuliwa kazi baada ya kuliongoza shirika hilo kwa miaka saba na anayechukua nafasi yake Ndagano kabla ya uteuzi huo alikuwa ni Makamu Mwenyekiti wa Mamlaka ya Usafariki wa Anga ya Rwanda,

Aidha uamuzi wa kumfukuza kazi Mirenge umekuja ikiwa ni siku moja tangu RwandAir kuzindua safari za Mumbai, India na mwezi ujao ikitaraji kuzindua safari za ndege za kwenda London, Uingereza.
Bosi RwandaAir atimuliwa kazi Bosi RwandaAir atimuliwa kazi Reviewed by Zero Degree on 4/08/2017 01:07:00 AM Rating: 5

Powered by Blogger.