Loading...

Alichoandika Waziri wa Mambo ya Ndani, Mwigulu Nchemba kuhusu Roma Mkatoliki

Usiku wa April 5 2017 taarifa za kukamatwa kwa msanii wa hip hop Roma Mkatoliki zilianza kuenea katika mitandao ya kijamii kwa kuandikwa kuwa Roma Mkatoliki na Moni wakiwa studio za Tongwe Records walikuja kukamatwa na watu wasiojulikana na kuwapeleka kusikojulikana.

Waziri wa Mambo ya Ndani ya Nchi Mwigulu Nchemba ambaye ndio anahusika na usalama wa raia, ametumia ukurasa wake wa instagram kuonesha kuguswa na tukio la kutekwa kwa Roma Mkatoliki na Moni, Waziri Nchemba ameeleza kuwa amewaagiza polisi kufuatilia na kutoa taarifa kwa umma.


“Nimeshtushwa kwa kutokuonekana kwa Msanii Roma na Wenzake mpaka sasa. Nimeshtuka zaidi nilipofuatilia na kuambiwa hakuna kituo chochote cha polisi kinachowashikilia. Nimeelekeza Polisi wafuatilie kwa karibu kujua undani wa tukio hili na hatima yao na kutoa taarifa kwa umma”
Alichoandika Waziri wa Mambo ya Ndani, Mwigulu Nchemba kuhusu Roma Mkatoliki Alichoandika Waziri wa Mambo ya Ndani, Mwigulu Nchemba kuhusu Roma Mkatoliki Reviewed by Zero Degree on 4/08/2017 01:08:00 AM Rating: 5

Powered by Blogger.