Loading...

Liverpool hatarini kumkosa Sadio Mane katika mechi zote zilizosalia

Mshambuliaji wa Liverpool Sadio Mane huenda asishiriki mechi saba za lig zilizosalia msimu huu kutokana na jeraha la goti.

Mane mwenye umri wa miaka 24 alitolewa uwanjani baada ya kugongana na Leighton Banes katika mechi ya ushindi wa 3-1 ya siku ya Jumamosi dhidi ya Everton.

Meneja Jurgen Klopp alisema kuwa ana hakika Mane alihitaji kufanyiwa upasuaji , hatua inayomfanya kuwa vigumu kushiriki katika mechi yoyote msimu huu.

Mchezaji huyo kutoka Southampton aliyesajiliwa kwa kitita cha pauni milioni 34 ameanzishwa mechi zote isipokuwa tano pekee za Liverpool msimu huu.

Kati ya mechi hizo tatu zilipata matkeo ya sare huku mbili zikipotezwa.

Liverpool iko katika nafasi ya tatu katika msimamo wa ligi huku zikiwa zimesalia mechi saba.
Liverpool hatarini kumkosa Sadio Mane katika mechi zote zilizosalia Liverpool hatarini kumkosa Sadio Mane katika mechi zote zilizosalia Reviewed by Zero Degree on 4/08/2017 01:13:00 AM Rating: 5

Powered by Blogger.