Loading...

Fabregas alivyoipita rekodi ya Frank Lampard wakati Chelsea ikiilaza Southamptoni jumanne

Cesc Fabregas sasa amefanikiwa kuipita rekodi ya mkongwe wa 'The Blues', Frank Lampard kwa kuweka rekodi yake ya kutoa 'assist' 103 katika ushindi wa goli 4-2 dhidi ya Southampton.

Muhispania huyo alitoa pasi ya juu kwa mchezaji mwenzake Diego Costa, pasi ambayo ilizaa matunda katika kipindi cha pili katika ushindi wa Chelsea kwenye uwanja wao wa Stamford Bridge katika wiki ya 34 ya Ligi kuu, ambayo hadi sasa vijana wa Antonio Conte wanaongoza kwa pointi saba zaidi.

Cesc kwa sasa amemwacha Lampard kwa zaidi ya 'assist' moja katika rekodi ya 
muda wote ya Ligi Kuu ya Uingereza.

Ryan Giggs bado anaongoza kwa kuweza kufikisha 'assist' 162 wakati akiwa na 'Red Devils', Fabregas naye ana mpinzani karibu kwa hivi sasa, ambaye ni nyota wa Manchester United, Wayne Rooney ambaye amepitwa 'assist' 2 tu na Cesc.


Orodha ya wachezaji 10 wenye assist nyingi zaidi katika Ligi kuu ya Uingereza:
  1. Ryan Giggs - 'assist' 162 
  2. Cesc Fabregas - 'assist'  103
  3. Frank Lampard - 'assist'  102
  4. Wayne Rooney - 'assist'  101
  5. Dennis Bergkamp - 'assist'  94
  6. Steven Gerrard - 'assist'  92
  7. David Beckham - 'assist'  80
  8. Teddy Sheringham - 'assist'  76
  9. James Milner - 'assist'  75
  10. Thierry Henry - 'assist'  74
Fabregas alivyoipita rekodi ya Frank Lampard wakati Chelsea ikiilaza Southamptoni jumanne Fabregas alivyoipita rekodi ya Frank Lampard wakati Chelsea ikiilaza Southamptoni jumanne Reviewed by Zero Degree on 4/28/2017 10:45:00 AM Rating: 5

Powered by Blogger.