Loading...

Walioghushi vyeti kutupwa jela miaka 7, hili ndilo jina la kwanza kutoka katika orodha

Waziri wa Utumishi, Angela Kairuki amemkabidhi Rais John Magufuli majina ya watumishi wenye vyeti feki huku akieleza kuwa waliobainika kughushi vyeti watahukumiwa kifungo cha miaka saba jela kulingana na kanuni za utumishi wa umma za mwaka 2016.

Kairuki amesema sheria hizo pia zinawaweka hatiani mawakala wote wanaotumika kutengeneza vyeti feki. 

Amesema kanuni za utumishi wa umma za 2016, zinaeleza kuwa muombaji wa nafasi za ajira serikali ni akitoa taarifa za uongo atachukuliwa hatua za kijinai na kinidhamu.


Baada ya kukabidhiwa ripoti hiyo, Rais alitaja jina la kwanza la mtu aliyetajwa kwenye ripoti hiyo. Alimtaja mtu huyo kuwa ni Abadallah Polea, ingawa hakueleza ni wa wapi na aliajiriwa katika sekta ipi ya umma.

Rais John Magufuli amesema watumishi 9732 waliobainika na vyeti feki wakatwe mshahara wa mwezi huu na wafukuzwe kazi na kisha wachukuliwe hatua kwa kufungwa jela miaka saba.

Amesema kwa kuwa watumishi hao wanajijua, hata majina yao yachapishwe kwenye magazeti kwa kuwa wameiibia serikali.

“Hawa ni majambazi, majizi kama yalivyo majizi mengine,.......” amesema
Walioghushi vyeti kutupwa jela miaka 7, hili ndilo jina la kwanza kutoka katika orodha Walioghushi vyeti kutupwa jela miaka 7, hili ndilo jina la kwanza kutoka katika orodha Reviewed by Zero Degree on 4/28/2017 01:34:00 PM Rating: 5

Powered by Blogger.