Loading...

Jinsi kifo cha wanandoa waliofariki wakipishana muda wa saa moja kilivyoshangaza wengi

Wanandoa Isaac Vatkin (91) na mkewe Teresa (89) waliofunga ndoa miaka 69 iliyopita wameishangaza dunia baada ya kufariki wakiwa wameachana kwa saa moja pekee.

Wawili hao, ambao walikuwa wakiishi katika eneo la Illinois mjini Chicago, walifariki Jumamosi iliyopita. Inadaiwa kuwa Teressa ndiye alikuwa wa kwanza kufariki dunia kwa ugonjwa wa Alzheimers, ambapo wote wawili walikuwa wakipata matibabu katika hospitali ya Highland Park Hospital.

Wakati Teressa anafariki dunia, mumewe Vatkin alikuwa amemshika mkono akiwa katika kitanda kilichokuwepo jirani na kile alicholala mkewe. Kwa mujibu wa wauguzi katika hospitali hiyo, dakika 40 baadae Issac alifariki dunia kwa tatizo la kushindwa kupumua vizuri.

Clara Gesklin ambaye ni mtoto wa wazee hao, ameiambia Daily Mail, “Upendo baina yao ulikuwa mkubwa sana, mmoja asingeweza kuishi bila mwenzake.”


Isaac Vatkin na Teressa enzi za uhai 
Jinsi kifo cha wanandoa waliofariki wakipishana muda wa saa moja kilivyoshangaza wengi Jinsi kifo cha wanandoa waliofariki wakipishana muda wa saa moja kilivyoshangaza wengi Reviewed by Zero Degree on 4/28/2017 01:47:00 PM Rating: 5

Powered by Blogger.