Emmanuel Adebayor amepata Hat-trick yake ya kwanza akiwa Istanbul
Mshambuliaji wa kimataifa wa Togo aliyewahi kuichezea Arsenal, Man City na Tottenham Hotspurs za England Emmanuel Adebayor ameirudisha timu yake ya Istanbul Basaksehir katika mbio za kuendelea kuwania Ubingwa wa Ligi Kuu Uturuki msimu huu kwa kuisaidia kuifunga Galatasaray usiku huu.
Adebayor ambaye alikumbwa na kipindi cha mpito na kuachwa na vilabu vya England amerudi katika kiwango na kuifungia timu yake hat-trick katika ushindi wa goli 4-0 wakiwa nyumbani katika uwanja wao wa Basaksehir Fatih Terim, Adebayor alifunga magoli kuanzia dakika ya 11 na dakika ya 44 na 57 akafunga magoli mawili ya kichwa.
Sare dhidi ya Karabukspor na kupoteza dhidi ya Akhisar Belediyespor kuliifanya Istanbul Basaksehir iachwe kwa point nane dhidi ya Besiktas wanaoongoza Ligi kwa point 61, hivyo hat-trick ya Adebayor katika ushindi wa goli 4-0 dhidi ya Galatasaray umefufua matumaini ya mbio za Ubingwa wakiwa wamebakia na michezo 7 Ligi Kuu ya Uturuki imalizike na wao wana point 56.
Sare dhidi ya Karabukspor na kupoteza dhidi ya Akhisar Belediyespor kuliifanya Istanbul Basaksehir iachwe kwa point nane dhidi ya Besiktas wanaoongoza Ligi kwa point 61, hivyo hat-trick ya Adebayor katika ushindi wa goli 4-0 dhidi ya Galatasaray umefufua matumaini ya mbio za Ubingwa wakiwa wamebakia na michezo 7 Ligi Kuu ya Uturuki imalizike na wao wana point 56.
Emmanuel Adebayor amepata Hat-trick yake ya kwanza akiwa Istanbul
Reviewed by Zero Degree
on
4/11/2017 01:43:00 AM
Rating: