Loading...

Hii ndio rekodi ya Pep Guardiola iliyovunjwa na Klabu ya Chelsea

Kipigo cha goli mbili kwa moja ambacho usiku wa kuamkia leo Chelsea iliifunga Manchester City kimeiwezesha klabu hiyo yenye makazi London kuendelea kupaa katika msimamo wa Ligi Kuu ya Uingereza.

Magoli ya Chelsea yalifungwa na Eden Hazard katika dakika ya 10 na 35 huku goli pekee la Man City likifungwa na Sergio Aguero katika dakika ya 26 ya mchezo huo ulipigwa Stamford Bridge.

Kipigo hicho kimevunja rekodi ambayo alikuwa ameiweka kocha wa Man City, Pep Guardiola ya kutofungwa katika michezo miwili mfululizo na timu moja kwa mchezo wa nyumbani na ugenini.

Matokeo ya michezo mingine ya EPL iliyopigwa usiku wa kuamkia leo ni:

  • Arsenal 3-0 West Ham
  • Hull City 4-2 Middlesbrough
  • Southampton 3-1 Crystal Palace
  • Swansea 1-3 Tottenham
  • Liverpool 2-2 Bournemouth
Msimamo wa Ligi Kuu ya Uingereza [EPL]:

Hii ndio rekodi ya Pep Guardiola iliyovunjwa na Klabu ya Chelsea Hii ndio rekodi ya Pep Guardiola iliyovunjwa na Klabu ya Chelsea Reviewed by Zero Degree on 4/06/2017 01:53:00 PM Rating: 5

Powered by Blogger.