Loading...

Hili ndilo lilikuwa jibu la Antonio Conte baada ya kuulizwa kama ana mpango wa kurejea Italia

Bosi wa 'The Blues', Antonio Conte alikiri kwamba anaweza kurejea Serie A.

Conte amekuwa akihusishwa na hoja ya kurejea Italia tangualipojiunga na 'The Blues', pamoja na fununu zilizopendekeza kuwa Inter Milan wana hamu sana ya kumshawishi meneja huyo ajiunge na San Siro kama kocha wao wa muda mrefu ili kuirejesha klabu mahali pazuri.

Muitaliano huyo mwenye umri wa miaka 47 hata hivyo, alikiri kwamba anaweza akashawishika kurejea nchini mwake katika siku zijazo na alieleza kuvutiwa na klabu za Inter na AC Milan, ambazo zote kwa sasa zina unafadhili wa wawekezaji wa Kichina.

Alipoulizwa kuhusu kuwa na mpango wa kuja kurejea nyumbani, Conte aliambia Televisheni ya Emigratis: "Ndiyo. Moyo wangu daima uko Italia. "

Wakati ilipokisiwa kuwa na mshahara wake ungekuwa mkubwa kwa kujiunga na klabu za Italia, alijibu kwa kuuliza swali hili: "Kwani si wamiliki wapya ndio na wao wameingia hivi karibuni?"
Hili ndilo lilikuwa jibu la Antonio Conte baada ya kuulizwa kama ana mpango wa kurejea Italia Hili ndilo lilikuwa jibu la Antonio Conte baada ya kuulizwa kama ana mpango wa kurejea Italia Reviewed by Zero Degree on 4/29/2017 03:14:00 PM Rating: 5

Powered by Blogger.