Loading...

Huu ndio utabili wa Jamie Carragher wa mechi ya Chelsea dhidi ya Man City jumatano

Carragher anauhakika 'The Blues' wataisambaratisha Manchester City siku ya jumatano usiku.

Chelsea bila shaka watakua na moto mkali wa hali ya juu kutokana na kipigo chao cha pili kwenye Ligi Kuu katika mechi 23 baada ya kupoteza kwa kichapo cha goli 2-1 dhidi ya Palace Jumamosi mchana, hivyo tutarajie kuoina Chelsea ikopambana ili kuokoa pointi tatu za mechi ijayo.

Blues walifanikiwa kupata goli lao kupitia kwa Cesc Fabregas katika dakika ya tano, Hata hivyo, Crystal Palace walikuwa washindi wa mechi hiyo kutokana na mabao ya Wilfried Zaha na Christian Benteke.

Vijana hao wa Antonio Conte, wanaongoza ligi kwa pointi saba zaidi ya Tottenham Hotspur walio katika nafasi ya pili baada Spurs kuibuka na ushindi wa goli 2-0 dhidi ya Burnley katika uwanja wa Turf Moor.

Chelsea itakuwa mwenyeji wa Manchester City walio nafasi ya nne katika Ligi Kuu siku ya Jumatano usiku kama ilivyo kwa upande wa vijana wa Pep Guardiola wanaotazamia kupunguza 'gape' lilipo kati yao na viongozi wa ligi hiyo.

Akizungumza na Sky Sports News HQ siku ya Jumatatu kuhusu pambano la Chelsea dhidi ya Manchester City, beki wa zamani wa Liverpool Carragher alisema:

"Uchezaji wao dhidi ya Palace utawapa kujiamini kuelekea katika mchezo wao katikati ya wiki dhidi ya Manchester City, kwa sababu utawafanya kujisikia bado wako katika kiwango kizuri, haikuwa kwamba ilikuwa mchezo mbaya.

"Bado wana nafasi nzuri, kuwa katika uwanja wa nyumbani dhidi ya Manchester City. Watu wengi watakuwa wakiangalia Chelsea kwa ukaribu zaidi katikati ya wiki hii, lakini nadhani kama watashinda mchezo huo, ni kama kumaliza kila kitu na kupumzika kitandani. Kushinda mchezo huo, na ni sawa na kubeba taji tayari. "
Huu ndio utabili wa Jamie Carragher wa mechi ya Chelsea dhidi ya Man City jumatano Huu ndio utabili wa Jamie Carragher wa mechi ya Chelsea dhidi ya Man City jumatano Reviewed by Zero Degree on 4/04/2017 01:40:00 PM Rating: 5

Powered by Blogger.