Loading...

Je, Nyota hawa kuihama Klabu ya Chelsea?

Ni lazima kwa namna yoyote ile vyombo vya habari kuwa na chochote cha kuandika, kwa kifupi ni kwamba havitaki kushindwa jambo.

Sasa badala ya kuripoti habari kwamba kuna mpanglo uliopo Chelsea wa kutaka kuwauza nyota wake wawili kwa mpigo [Hazard na Costa] tofauti na uvumi kuhusu uhamisho kama ilivyofanyika katika kipindi cha miezi sita iliyopita, wameamua kuitoa habari kamili.

Leo tuna habari zilizotawala katika vyombo vya habari vingi zinazodai kuwa nyota wakuu wa Chelsea, Eden Hazard na Diego Costa wataondoka Chelsea.
Utaipenda hii, vyombo vya habari vinasema kwamba Real Madrid bado wanamhitaji Eden Hazard na wako tayari kumsajili endapo yeye mwenyew yuko tayari kujiunga na klabu hiyo.

Na Costa, inadaiwa pia anataka kuondoka, kwani inasemekana kuwa hivi karibuni alisema kwamba hali ya hewa imemuwea mbaya kwake. Lakini hizo ni taarifa tu, zinaweza kuwa za kweli au uongo.

Habari yenye ukweli halisi kutoka Chelsea
 ziko hivi, Hazard kwa upande wake katika mahojiano ya hivi karibuni na waandishi wa habari alisema  kwamba anafuraha kuwa na klabu ya Chelsea na kimsingi ni majeruhi hadi hivi sasa kulingana na uvumi utokao ndani ya klabu.

Costa naye alisema ana furaha sana kuwa 'The Blues' ilam tu ana masuala mengine binafsi yanayohusiana na maisha yake ya London.

Ni habari za kupita tu na vyombo vya habari kwa hilo vinasema uongo.
Je, Nyota hawa kuihama Klabu ya Chelsea? Je, Nyota hawa kuihama Klabu ya Chelsea? Reviewed by Zero Degree on 4/11/2017 04:26:00 PM Rating: 5

Powered by Blogger.