Loading...

Jinsi Pempasi zinavyowasabishia watoto wadogo ugonjwa wa Figo

KITENDO cha kumwacha mtoto muda mrefu akiwa amevaa pempasi, kinaweza kumsababishia ugonjwa wa UTI na figo.

Kauli hiyo ilitolewa Dar es Salaam hivi karibuni na bingwa wa magonjwa ya watoto katika Hospitali ya Taifa Muhimbili (MNH), Dk. Gudila Valentine, alipofanya mahojiano na gazeti hili.

Dk. Gudila alisema mtoto atapata maambukizi pindi atakapojisaidia na kukaa muda mrefu na nepi au pempasi.

Alisema kinyesi hicho kinakuwa kinarudi kuelekea katika njia ya mkojo.

“Bakteria anayesababisha UTI anaishi katika sehemu ya haja kubwa, kwa hiyo lazima mtoto naye asafishwe mara kwa mara kama ilivyo kwa watu wazima ili kumkinga dhidi ya maambukizi ya ugonjwa huu.

“Lazima usafi uwe kitu cha kwanza. Kwa kuwa bakteria yupo kwenye kinyesi, kinapokaa pale kwa muda mrefu, hasa akiwa ni mtoto wa kike, kinapata nafasi ya kupanda na kurudi kwenye njia ya mkojo kwa sababu zile njia zimekaa karibu karibu, hivyo inakuwa rahisi kwa yeye kupata UTI,” alisema Dk. Gudila.

Pia alisema ndiyo maana wazazi wanashauriwa wasafishe na kubadilisha nepi au pempasi mara kwa mara kwa kuwa usafi ni suala la msingi na watoto wakubwa wasafishwe kutoka mbele kwenda nyuma.

Alisema kuna watu wanafikiria kwamba watoto hawawezi kuugua magonjwa ya figo kama ilivyo kwa watu wazima jambo ambalo si kweli.
Jinsi Pempasi zinavyowasabishia watoto wadogo ugonjwa wa Figo Jinsi Pempasi zinavyowasabishia watoto wadogo ugonjwa wa Figo Reviewed by Zero Degree on 4/06/2017 10:42:00 AM Rating: 5

Powered by Blogger.