Loading...

Korea Kaskazini yapewa onyo juu ya majaribio ya makombora

Mataifa mawili ya bara la Asia, yametoa onyo kali dhidi ya utawala wa Pyongyang, kwamba itaadhibiwa vikali, iwapo itadhubutu tena kufanya majaribio ya zana zake za kinuklia.

Mataifa hayo, Korea Kusini na China, yamedai yatachukua hatua kali dhidi ya Korea Kaskazini, ikiwa itafanya majaribio ya zana zake za kitonoradi zinazovuka mipaka ya kimataifa.

Tangazo hilo limetoka baada ya mkutano uliofanyika Seoul, kati ya wajumbe wa China na Korea Kusini, na hatua ya Marekani ya kutumameli za kivita hadi katika maeneo ya maji kwenye rasi ya Korea.

Taifa la Korea Kaskazini mara kwa mara limekuwa likiimarisha uwezo wake wa kivita, licha ya kuwekewa vikwazo na Umoja wa mataifa.

Kwa kweli, majaribio hayo ya mara kwa mara, yameongezeka sana chini ya utawala wa Rais Kim Jong-un.

Rais Trump wa Marekani, ameahidi "kutanzua" Korea Kaskazini bila ya kusaidiwa na China, mshirika wa pekee wa Pyongyang.
Korea Kaskazini yapewa onyo juu ya majaribio ya makombora Korea Kaskazini yapewa onyo juu ya majaribio ya makombora Reviewed by Zero Degree on 4/10/2017 06:36:00 PM Rating: 5

Powered by Blogger.