Loading...

Jinsi biashara za barabarani zinvyowagharimu wananchi wanaotembea kwa miguu

WATEMBEA kwa miguu katika manispaa ya Dodoma wameziomba mamlaka husika kuingilia kati suala la wafanyabiashara kupanga bidhaa zao njiani kwani inasababisha usumbufu kwa watumiaji wa njia hizo.

Wakizungumza kwa nyakati tofauti walisema kumezuka mtindo wa wafanyabiashara wa vyakula, nguo na viatu kupanga chini bila kuacha maeneo ya wapita kwa miguu.

Mkazi wa Kisasa, Hadija Msulami alisema kuanzia stendi kuu ya mabasi kuelekea kituo cha daladala Jamatini kumekuwa na utitiri mkubwa wa wafanyabiashara na hivyo kukosesha hata mahali salama pa kupita hivyo wengi kupita kando ya barabara.

“Ni shida kubwa hapa ukitaka kupita njia hii unafikiria hasa hapa nje ya uwanja wa Mashujaa kila mtu kapanga bidhaa hakuna pa kupita,“ alisema.

Alisema ni vyema kama mamlaka husika zikaelekeza mahali wanapotakiwa kupanga biashara iwe hata pembeni ya eneo hilo na si kuweka katikati ya njia.

Mmoja wa wafanyabiashara katika soko kuu la Majengo, Ramadhani Muzazi alisema kumekuwa na wimbi kubwa la wafanyabiashara kupanga bidhaa kando ya barabara nje ya masoko, hali ambayo inaathiri vipato vya wanaolipa kodi.

“Hao hawatoi ushuru, holela nayo ina unafuu wake wateja wengine wanaishia nje hawaingii ndani wanaathiri mapato ya wafanyabiashara wanaolipa kodi,” alisema.

Alisema sasa ifike mahali serikali ikapata ufumbuzi wa kudumu ili wanaofanya biashara holela wakae kwenye maeneo maalumu, hasa wakati huu ikizingatiwa Dodoma imekuwa makao makuu ya nchi.

Mkurugenzi wa Manispaa ya Dodoma, Godwin Kunambi hakupatikana kuzungumzia suala hilo.
Jinsi biashara za barabarani zinvyowagharimu wananchi wanaotembea kwa miguu Jinsi biashara za barabarani zinvyowagharimu wananchi wanaotembea kwa miguu Reviewed by Zero Degree on 4/10/2017 06:12:00 PM Rating: 5

Powered by Blogger.