Loading...

Nape aeleza maana ya kupita migongoni mwa wananchi wake

Mbunge wa Mtama, Nape Nnauye akilia huku akipita juu ya migongo ya wananchi wake
Mbunge wa jimbo la Mtama, Nape Moses Nnauye amefunguka kuhusu kitendo alichofanyiwa na wananchi wa jimbo lake kwa kulala chini na kutengeneza barabara huku wakimtaka na yeye apite juu yao kwa kuwakanyaga.

Mapokezi hayo ambayo yameonekana yalikuwa kama ya kifalme yaliliza mbunge huyo ambaye aliwahi kuwa waziri wa Habari, Utamaduni, Sanaa na Michezo kabla hajaondolewa kwenye kiti hicho mwezi uliopita na Rais Magufuli na nafasi yake kuchukuliwa na Dkt Harrison Mwakembe.

Nape ametoa ufafanuzi huo kupitia mtandao wa Twitter kwa kuandika, “Kwa mila za kusini tendo hili ni la heshima KIMILA na ukikataa ni sawa na DHARAU KUBWA kwa waliokufanyia, hata hivyo ndio maana NILILIZWA!.”

Wikiendi hii Nape alifanya mikutano miwili jimboni kwake.
Nape aeleza maana ya kupita migongoni mwa wananchi wake Nape aeleza maana ya kupita migongoni mwa wananchi wake Reviewed by Zero Degree on 4/10/2017 05:37:00 PM Rating: 5

Powered by Blogger.