Loading...

Kumbe Korea Kaskazini ilifanya maonyesho ya Silaha Bandia!

Maonyesho ya kijeshi mjini Pyongyang yaliyoonyeshwa duniani kote
Korea kaskazini inaluamiwa kwa kuonyesha silaha bandia katika maonyesho ya hivi majuzi ya ubabe wake wa kijeshi.

Afisa wa zamani wa masuala ya ujasusi anasemna baadhi ya bunduki na makombora yaliyotumiwa kwenye maonyesho hayo yalikuw bandia.

Michael Pregent alikiambia kituo cha runinga cha Fox kuwa baadhi ya bunduki zilizokuwa kwenye maonyesho hayo zilikuwa ni za kujekesha.

Lakini maonyesho kama hayo kuonyesha ubabe wa kijeshi yametumiwa kwa miongo kadhaa.

Kwa sasa msukosuko ni mkubwa kati ya Marekani na Korea Kaskazini.

Hii ni baada ya rais wa Marekani kuapa kuwa ni lazima atakabiliana na tisho la Korea Kaskazini.

"Sio kuwa Korea kaskazini inafikiri kuwa itashinda Marekani lakini kile ambacho itafanya ikiwa itashambuliwa," bwana Pregent alisema.

Silaha hizi bandia zilitengenezwa kukwepa mashambulizi ya angani na kuwachanganya marubani wa jeshi kushambulia vifaru bandia baada ya vifaru halali

Wasanii ya jeshi la Ufaransa nao walichora mito bandia na mitaro ili kuwachanganya marubani wa ndege za vita.

Ujanja kama huo pia ulitumiwa wakati wa vita vya pili vya Dunia.

Miongo kadha kabla miti ilitumika kupigana katika vita vya wenyewe nchini Marekani

Miti hii ilipakwa rangi hadi kifanana na silaha ya kurusha makombora.

Lengo lilikuwa ni kuwachanganya maadui kuhusu ni wapi kulikuwa na adui.

Aina hii ya silaha bandia zilitumika karne za 18 na 19

Picha hii inaonyesha wanajeshi wa Ujerumani wakikimbia ndani ya vifaru bandia miaka ya 1920.
Kumbe Korea Kaskazini ilifanya maonyesho ya Silaha Bandia! Kumbe Korea Kaskazini ilifanya maonyesho ya Silaha Bandia! Reviewed by Zero Degree on 4/28/2017 02:37:00 PM Rating: 5

Powered by Blogger.