Loading...

VIDEO: Kisa cha shabiki wa Spurs kupigwa na mashabiki wenzake akidhaniwa kuwa ni mamluki

Shabiki wa klabu ya Tottenham Hotspurs, Michael Voller, amevamiwa na kundi la mashabiki wa timu yake na kuumizwa vikali baada ya mashabiki wa timu hiyo kudhani kuwa ni shabiki wa klabu ya Chelsea.

Madaktari wanahofu juu ya shabiki huyo wa klabu ya Tottenham Hotspurs kuweza kupoteza uwezo wake wa kuona baada ya majeraha yake kuwa makubwa zaidi katika sehemu za ndani ya Macho yake. Kufuatia vurugu hizo, Askari Polisi wanaamini kuwa mashabiki wenzake walikosea wakidhani ni shabiki wa klabu ya Chelsea.

Michael Voller
Michael Voller alishambuliwa baada ya timu yake kushindwa katika mchezo wa nusu fainali ya kombe la FA dhidi ya Chelsea, mchezo uliochezwa siku ya Jumamosi katika uwanja wa Wembley.

Shabiki huyo, kabla ya kufikwa na mkasa huo, alikuwa katika Mgahawa wa Indian, uiopo nje ya uwanja huo ndipo akapigwa ngumi ya uso iliyompelekea kupata maaumivu makali na kuvunjika kwa baadhi ya sehemu za mifupa yake, pamoja na sehemu za macho.


VIDEO: Kisa cha shabiki wa Spurs kupigwa na mashabiki wenzake akidhaniwa kuwa ni mamluki VIDEO: Kisa cha shabiki wa Spurs kupigwa na mashabiki wenzake akidhaniwa kuwa ni mamluki Reviewed by Zero Degree on 4/28/2017 02:54:00 PM Rating: 5

Powered by Blogger.