Loading...

Mali inayomilikiwa na Ivanka Trump pamoja na mumewe yawekwa hadharani

Ikulu ya Marekani, imetoa maelezo kuhusu mali ya binafsi ya watu waliomo katika serikali ya Rais Donald Trump.

Mali hiyo imedhihirishwa kama sheria inavyoelekeza, na inaonyesha kuwa mtoto wa rais wa kike, Ivanka pamoja na mumewe, wana kama dola milioni 740.

Piya imetangazwa kuwa mshauri mkuu wa rais kuhusu uchumi, Gary Cohn, ana kama dola robo bilioni.

Ikulu ya White House inajaribu kuonyesha kuwa watu katika serikali ya Trump wanajiweza, na inasema watu hao wamejitolea sana kwa kukubali kutumika serikalini.

Watu walio kwenye baraza la mawaziri la bwana Trump wana jumla ya mali ya dola bilioni 12.
Mali inayomilikiwa na Ivanka Trump pamoja na mumewe yawekwa hadharani Mali inayomilikiwa na Ivanka Trump pamoja na mumewe yawekwa hadharani Reviewed by Zero Degree on 4/01/2017 05:56:00 PM Rating: 5

Powered by Blogger.