Loading...

Maonyesho ya Utalii Tanzania sasa kufanyika Afrika Kusini

Mkurugenzi Mtendaji wa kampuni ya Kili Fair inayoendesha maonyesho hayo, Tom Kunkler.
MAONYESHO ya Kimataifa ya Utalii Tanzania (Kili Fair) mwaka huu yatafanyika katika jiji la Cape Town, nchini Afrika Kusini Aprili 19 hadi 21 mwaka huu.

Maonyesho hayo pia yatatumika kuutangaza ipasavyo Mlima Kilimanjaro na kutoa elimu kwa wageni kutoka nchi mbalimbali duniani kuhusu fursa za kibiashara katika sekta ya utalii nchini.

Akizungumza mwishoni mwa wiki, Mkurugenzi Mtendaji wa kampuni ya Kili Fair inayoendesha maonyesho hayo, Tom Kunkler, alisema kazi ya kuwasilisha muundo na mpango kazi wa maonyesho hayo kwa mwaka 2017 kwa lengo la kuvutia wawekezaji na wadau wa utalii pia itafanyika nchini humo.

“Tunavuka mipaka ya nchi na kwenda kutangaza utalii wa Tanzania nje kwa sababu sekta hiyo ndiyo kichocheo kikubwa cha ukuaji wa uchumi. Tunawakaribisha watu wa utalii wa Afrika ya Kusini kuitembelea Tanzania ili kuchochea ukuaji wa sekta nyingine za kiuchumi kama viwanda, biashara, kilimo na usafirishaji,” alisema Tom.

Kwa hapa nchini, maonyesho hayo kwa mwaka huu yatafanyika mjini Moshi kati ya Juni 2 hadi 4 katika viwanja vya Chuo Kikuu cha Ushirika (MoCU).

Tangu kuanzishwa kwa maonyesho hayo miaka mitatu iliyopita, Kili Fair imepata mafanikio makubwa kutokana na kuunufaisha kiuchumi mkoa wa Kilimanjaro na taifa kwa ujumla, huku ukitoa fursa ya kuitangaza utalii nchini kimataifa.

Zaidi ya washiriki 300 kutoka nchi nane duniani watashiriki maonyesho hayo ambayo yameorodheshwa kwenye Mtandao wa Masoko wa WTM Afrika ambao unaoziunganisha nchi za Jumuiya Afrika Mashariki na Afrika Kusini.

Source: Nipashe
Maonyesho ya Utalii Tanzania sasa kufanyika Afrika Kusini Maonyesho ya Utalii Tanzania sasa kufanyika Afrika Kusini Reviewed by Zero Degree on 4/03/2017 11:49:00 AM Rating: 5

Powered by Blogger.