Loading...

Miezi mitatu baada ya kujifungua mtoto wa kwanza, Janet Jackson [50] aachana na mume wake

Miezi michache tu baada ya kupata mtoto wake wa kwanza akiwa na umri wa miaka 50, Janet Jackson ameachana na mume wake bilionea Wissam Al Mana.

Japo vyanzo vimesema wameachana kwa kukubaliana na kwamba watashirikiana kumlea mtoto wao wa kiume, vingine vinasema hawakuwa na maelewano kwa muda.

“Aliona [Wissam] amekuwa muamrishaji sana pindi cha ujauzito wake [Janet] na alikuwa ameshamruhusu kumwamulia muonekano wake na hata jinsi alivyotumbuiza kwenye matamasha,” chanzo kinachofanya kazi na wapenzi hao kilisema.

Janet pia aliacha kufanya video alizikuwa amezoea na hivyo kuhusu anaendelea kupoteza mashabiki wake. Kingine, Jackson alikuwa hapendezwi na kujitenga kwa mume wake, ambaye alikuwa akikutana na ndugu zake kwa nadra sana na pia kutoonesha kuwajali kwenye matatizo.

Walipata mtoto wao, Eissa Al Mana, January 3 ikiwa ni miaka mitano tangu wafunge ndoa.
Miezi mitatu baada ya kujifungua mtoto wa kwanza, Janet Jackson [50] aachana na mume wake Miezi mitatu baada ya kujifungua mtoto wa kwanza, Janet Jackson [50] aachana na mume wake Reviewed by Zero Degree on 4/10/2017 09:39:00 AM Rating: 5

Powered by Blogger.