Loading...

Askofu Gwajima amvaa Halima Mdee

Mbunge wa Kawe, Halima Mdee.
ASKOFU wa Kanisa la Ufufuo na Uzima, Josephath Gwajima, amemshauri Mbunge wa Kawe, Halima Mdee, kusimama mbele ya Bunge kumuomba msahama Spika wa Bunge, Job Ndugai kwa kumrushia lugha ya matusi siku ya mchakato wa uchaguzi wa wabunge wa Bunge la Afrika Mashariki.

Askofu Gwajima alitoa kauli hiyo jana wakati akihubiri katika ibada ya kanisa hilo, Ubungo jijini Dar es Salaam.

Hata hivyo, Mdee ambaye ni mbunge wa jimbo hilo kupitia Chama cha Demokrasia na Maendeleo (Chadema), hakumtukana Spika na ameshahojiwa na Kamati ya Haki, Maadili na Madaraka ya Bunge.

Mdee alishitakiwa kwa makosa mawili: kusema bungeni bila idhini ya Spika na kutoa lugha ya matusi, kuudhi na kudhalilisha mbunge mwingine.

Gwajima ambaye pia alitaja watu anaoamini kuwa ndiyo walimteka msanii wa muziki wa kizazi 'Roma Mkatoliki' Alhamisi, alisema Mdee ni mwakilishi wa wananchi hivyo anapaswa kuwa mfano wa kuigwa.

“Mdee mimi ni mbunge wangu na ni rafiki yangu, lakini kwa kauli ya kumtukana matusi Spika siwezi kumuunga mkono, anapaswa kuomba msamaha,” alisema Askofu Gwajima.

“Hatuwezi kuwakemea watu wengine ambao wanakosea halafu na yeye tukamuacha, katika hili kwa kweli hakufanya vizuri anapaswa kwenda kuomba msahama.

"Yeye ni mwakilishi wa wananchi kwa hiyo anapaswa kuwa mfano wa kuigwa, na asipoomba msamaha, Jumapili ijayo ‘nitampiga’.”

Source: Nipashe
Askofu Gwajima amvaa Halima Mdee Askofu Gwajima amvaa Halima Mdee Reviewed by Zero Degree on 4/10/2017 09:51:00 AM Rating: 5

Powered by Blogger.