Loading...

Mshike mshike wa kuwania ubingwa wa Ligi kuu ya Uingereza kuendelea tena Leo

Ligi kuu ya England [EPL] itaendelea tena leo kwa mchezo mmoja kupigwa kati ya vinara wa ligi hiyo Chelsea ambao watakua katika uwanja wao wa nyumbani kuwaalika Southampton leo usiku Saa tatu na dakika 45.

Nahodha wa Chelsea Gary Cahill anatarajiwa kuwa sehemu ya kikosi baada ya kurejea mazoezini tangu kupona tatizo la tumbo.



Diego Costa na Eden Hazard wanatarajiwa kuanza katika mchezo huu baada ya kuanzia benchi katika mchezo wa kombe la FA dhidi ya Tottenham wikiendi iliyopita.

Kiungo wa Southampton Oriel Romeu amereje kwenye kikosi cha timu yake baada ya kufungiwa michezo miwili iliyopita, Sam McQueen, Aust C, McCarthy A, pamoja van Dijk V wataukosa mchezo huo wakisumbuliwa na majeraha.

Chelsea wanaongoza ligi kwa pointi 75 wakiwa wamecheza michezo 32 wakifuatiwa na Tottenham wenye pointi 71 kwa michezo 32 pia.
Mshike mshike wa kuwania ubingwa wa Ligi kuu ya Uingereza kuendelea tena Leo Mshike mshike wa kuwania ubingwa wa Ligi kuu ya Uingereza kuendelea tena Leo Reviewed by Zero Degree on 4/25/2017 12:06:00 PM Rating: 5

Powered by Blogger.