Loading...

Mwezi mmoja baada ya kutimuliwa upinzani, Tshibala ateuliwa kuwa Waziri mkuu DRC

Rais wa Jamhuri ya Kidemokrasi ya Congo, Joseph Kabila, amemteua Bruno Tshibala kuwa Waziri Mkuu mpya katika Serikali ya kugawana madaraka.

Bwana Tshibala ataongoza taifa hilo hadi uchaguzi wa Urais unaotazamiwa kufanywa baadaye mwakani.

Bruno Tshibala ndiye waziri mkuu mpya DR Congo
Alitimuliwa kutoka chama kikuu cha upinzani, UDPS, mwezi uliopita baada ya kupinga watu waliochaguliwa chamani kuchukua madaraka ya kiongozi aliyefariki Februari, Etienne Tshisekedi.

Waandishi wa habari wanasema kuwa kuchaguliwa kwa Bwana Tshibala kutawagawanya zaidi wapinzani wa Bwana Kabila baada ya mashauriano ya kujadili jinsi atakavyoondoka mamlakani kuporomoka juma lililopita.
Mwezi mmoja baada ya kutimuliwa upinzani, Tshibala ateuliwa kuwa Waziri mkuu DRC Mwezi mmoja baada ya kutimuliwa upinzani, Tshibala ateuliwa kuwa Waziri mkuu DRC Reviewed by Zero Degree on 4/08/2017 01:41:00 PM Rating: 5

Powered by Blogger.