Loading...

VIDEO: Alichosema Kamanda Sirro leo hii kuhusu sakata la kutekwa kwa akina ROMA

Kamanda wa Polisi Kanda Maalum ya Dar es Salaam, Kamishna Simon Sirro amesema kuwa, tukio la kutekwa kwa msanii ROMA Mkatoliki, na wenzake watatu usiku wa kuamkia juzi, Polisi Dar imeunda kikosi maalum cha upelelezi na wanaendelea na kazi mpaka sasa.

Sirro amesema hayo leo wakati akizungumza na wanahabari Makao Makuu ya Polisi Dar ambapo amewataka Watanzania waendelee kutoa ushirikiano kwa Polisi ili kufanikisha kupatikana kwa watu hao.



Sirro amefunguka haya;

“Matukio ya utekaji hayajaanza leo, yamekuwepo na tukafanyakazi tukapata majibu. Tukio hili la kutekwa wasanii ni la kawaida.


“Tukio hili la utekaji ni kama matukio mengine ya uhalifu ambayo tumeyashungulikia, hatuwezi kusema hali mbaya kwa tukio hili.

“Mimi ni Kamishna wa Polisi siwezi kusema wasanii watapatikana lini, kama kuna kiongozi alitaja siku watakayopatikana, muulizeni yeye.




“Upelelezi ndio utakao amua hawa watu watapatikana lini. Tunafanya kazi kufuata taaluma ni si kutoa maneno tu.

“Wanaosema simu ya Roma ilikuwa inapatikana na kuhoji kwanini hatukwenda TCRA, wasitufundishe kazi, wamejuaje hatukwenda TCRA?

“Wengine walalamika wasema leo ni siku ya tatu tumechelewa kutoa majibu walipo, wajue majibu ya polisi kuuawa tulipata baada ya mwezi mmoja.

“Hawa watu hawakuja kuniambia kuwa Kamishna Sirro sasa tunakwenda kuwateka, kwamba ninajua walipo lakini sitaki kuwakamata.

Msikileze kamanda siro hapo chini: 

VIDEO: Alichosema Kamanda Sirro leo hii kuhusu sakata la kutekwa kwa akina ROMA VIDEO: Alichosema Kamanda Sirro leo hii kuhusu sakata la kutekwa kwa akina ROMA Reviewed by Zero Degree on 4/08/2017 02:13:00 PM Rating: 5

Powered by Blogger.