Loading...

Roma na wenzake wapatikana wakiwa salama

Taarifa zilizotufikia zimedai kuwa Roma na watu wengine waliokuwa wameshikiliwa tangu Jumatano hii wamepatikana wakiwa salama.

Kaka wa Roma, Omar Musa amesema Roma alirudishwa nyumbani leo, na kwa sasa yupo kituo cha Oyesterbay. 

Hata hivyo Omar hakutaka kueleza kwa kina kuhusu kurejea kwa Roma akisema kuwa hadi familia itakapotoa tamko.



Mkuu wa polisi (OCD) wilaya ya Kinondoni, Abubakar Kunga amethibitisha kupatikana kwa wote waliopotea. Lakini kwa sasa amesema wanafanya nao mahojiano ya kipolisi katika kituo cha Oysterbay lakini baada ya muda mfupi wataongea na waandishi ili kutoa taarifa kamili.

Kupatikana kwao kumefuatia wito mkubwa uliokuwa ukipaishwa na wasanii wenzake na mashabiki kuhusu kuachiliwa huru.

Awali, Kamanda wa Polisi Kanda Maalum ya Dar es salaam, Kamishina Simon Sirro alisema bado walikuwa wakiendelea na upelelezi wa tukio la kupotea (kutekwa) kwa msanii Roma Mkatoliki na wenzake.

Akiongea na waandishi wa habari mchana huu Polisi Central jijini Dar es salaam, Kamanda Sirro alisema tukio la utekwaji wa Roma na wenzake ni aina ya matukio ambayo hutokea mara kwa mara.

“Matukio ya utekaji hayajaanza leo, hili la kina Roma na wenzake ni tukio kama matukio mengine yaliyokuwa ya ujambazi kwahiyo tupeni muda tupeleleze, tukifika mahali pazuri tutawaita tuwape taarifa lakini nimeona mitandao mingi inazungumza, jana nikaona wasanii wamekutana lakini nikajiuliza hivi yangekuwa haya matukio yanatokea ya uhalifu yanapotokea watu wanakutana ingekuwaje?,” alisema Sirro.

Aliongeza, “Jamani kazi hii tumepewa kwa mujibu wa Katiba na ni lazima tutimize wajibu wetu kwa hiyo tupeni muda tutakuwa na majibu mazuri katika hili,” aliongeza.
Roma na wenzake wapatikana wakiwa salama Roma na wenzake wapatikana wakiwa salama Reviewed by Zero Degree on 4/08/2017 04:05:00 PM Rating: 5

Powered by Blogger.