Loading...

Kauli ya Conte juu ya tetesi zinazodai kuwa ana mpango wa kumsajili Andrea Pirlo

Andrea Pirlo alihusishwa na kuhamia Chelsea kama kocha msaidizi na aliyekuwa kocha wa zamani wa Chelsea, Ray Wilkins wakati wa mahojiano na TALKSPORT.

Hata hivyo habari hizo zinageuka na kuwa za uongo.

Kiungo huyo wa New York City FC mara ya mwisho alikuwa akihusishwa na kazi mpya Chelsea kwa ajili ya kujaza nafasi ya kocha msaidizi aliyeondoka Stamford Bridge, hata hivyo, bosi wa 'The Blues' kwa mara nyingine tena ameviambia vyombo vya habari kwamba habari zilitawala hivi sasa si za ukweli bali ni habari za uongo na za kutengeneza.

Conte alisisitiza kuwa sula la Pirlo kuja Chelsea ni gumu, ambaye kwa sasa ni mchezaji katika Klabu ya MLS ya New York, na bado anataka kuendelea na kazi yake ya kucheza mpira.

Kocha wa Chelsea alisema: "Naendelea kusikiliza mambo mengi [juu ya kujaza nafasi ya Steve Holland]. Hii ni moja ya habari za ajabu sana kwa sababu Pirlo bado anachezea MLS na bado anataka kuendelea kucheza.


"Sijui kwa nini mtu anataka kuniweka katika hali hii. Ni jambo la kawaida kwangu lakini ni cha muhimu ni kuwa makini na linalotuzonga kwa sasa, mimi na wachezaji wangu.

"Kinachotukabili sasa ndicho cha muhimu zaidi kuliko cha wakati ujao. Nataka kumaliza msimu huu kwa mafanikio makubwa, si tu kuishia kuuita moja ya msimu mzuri pekee."
Kauli ya Conte juu ya tetesi zinazodai kuwa ana mpango wa kumsajili Andrea Pirlo Kauli ya Conte juu ya tetesi zinazodai kuwa ana mpango wa kumsajili Andrea Pirlo Reviewed by Zero Degree on 4/08/2017 11:36:00 PM Rating: 5

Powered by Blogger.