Loading...

Nay wa Mitego azua gumzo kwa mashabiki baada ya kuandika ujumbe huu Instagram

Nani kamtibua tena Nay wa Mitego? Kupitia mtandao wa Instagram rapper huyo ameandika ujumbe ambao umeonekana kuibua maswali mengi kwa mashabiki.

Kupitia mtandao huo Nay ameandika maneno mazito ambayo inaonekana amekerwa na kitendo kinachoonekana kufanywa na rafiki yake ambaye pia ni msanii japo hajamtaja jina mtu huyo.

Kutokana na ujumbe huo inaonekana kitendo hicho kilichomkera Nay kimetokanana hili jambo linaloendelea kwa sasa kati ya muziki na siasa.

 “1: Unatuchezea Sinema mpaka wana.?! F***k.! Njaa zitatuua.
#Wapo️,” ameandika Nay katika mtandao huo.

2: Una Sign mkataba wa kucheza Sinema yenye Quality Mbovu, Tena inayo Rekodiwa kwa Camera ya Simu.?! Unategemea nini.? Nakuvua vyeo ata Kama Mkataba ni Mnono, ItakuCost tu na utayumbisha Career yako.!
Mwana Katoa Bokoo.!,” ameongeza.
Nay wa Mitego azua gumzo kwa mashabiki baada ya kuandika ujumbe huu Instagram Nay wa Mitego azua gumzo kwa mashabiki baada ya kuandika ujumbe huu Instagram Reviewed by Zero Degree on 4/10/2017 12:19:00 PM Rating: 5

Powered by Blogger.