Loading...

Ndege zisizo na rubani zaanza kusaka mifugo iliyofichwa kwenye maeneo ya hifadhi mkoani Kagera.

Kikosi kinachoendesha operesheni maalumu katika mkoa wa Kagera ya kuhakikisha kinabaini na kuikamata mifugo yote iliyoko kwenye maeneo ya hifadhi ya misitu na mapori ya akiba kimeanza kuendesha operesheni hiyo kwa kutumia ndege zisizo na rubani ambazo zitazunguka kuisaka mifugo iliyofichwa katika baadhi ya maeneo yafikika kwa urahisi yaliyoko kwenye mapori ya Nyantakala,Kimisi, Burigi na Biharamulo.

Ndege hizo zisizo na rubani zimerushwa angani na kikosi hicho kutokea katika kambi ya kituo kiteule kilichoko katika hifadhi ya msitu wa Nyantakala na zimeanza kazi ya kuisaka mifugo iliyofichwa katika maeneo ya msitu huo ulioko wilayani Biharamulo, Peremela Paranjo ambaye ni afisa wanyamapori toka mapori ya Lukwika na Lumesule yaliyoko wilayani Mtwara anayeongoza ndege hizo akizungumza amesema zinauwezo wa kusafiri umbali mrefu hivyo zitasaidia kuyabaini makundi ya mifugo yaliyofichwa kwa kuyapiga picha.

Wakati huo huo, kufuatia operesheni hiyo, baadhi ya wafugaji waliozungumza ambao uuza mifugo yao katika mnada wa Rusaunga ulioko wilayani Biharamulo wamesema bei ya uuzaji wa ng’ombe imeshuka sana kwa kuwa mifugo inayoletwa katika mnada huo ni mingi sana na wameeleza kuwa inato hatua ya baadhi ya wafugaji ya kutaka kupunguza mifugo waliyonayo baada ya kuondolewa kwenye hifadhi ya misitu na mapori ya akiba huku baadhi ya wanunuzi wa mifugo wakielezea kuwa hiyo ni faraja kwao.
Ndege zisizo na rubani zaanza kusaka mifugo iliyofichwa kwenye maeneo ya hifadhi mkoani Kagera. Ndege zisizo na rubani zaanza kusaka mifugo iliyofichwa kwenye maeneo ya hifadhi mkoani Kagera. Reviewed by Zero Degree on 4/07/2017 02:05:00 PM Rating: 5

Powered by Blogger.