Loading...

BreakingNews: Kampuni ya China yainunua rasmi klabu ya AC Milani ya Italia

Timu ya soka ya AC Milan ya Italia imeuzwa kwa kampuni moja ya Uchina na kufikia kikomo cha umiliki na aliyekuwa Waziri Mkuu wa nchi Italy na tajiri Silvio Berlusconi.

Tajiri Silvio Berlusconi

Kampuni ya China Rossoneri Sport Investment Lux, imekamilisha mkataba wa kuinunua timu hiyo kwa kima cha dola milioni 628, huku ikiwa na matumaini ya "kuongeza faida mara dufu".

Klabu hiyo ya Serie A imekuwa chini ya umiliki wa bilionea Silvio Berlusconi, tangu mwaka 1986.

Katika kipindi hicho chote, AC Milan ilifaulu kunyakua mataji manane katika ligi kuu na kunyakuwa kombe la klabu bingwa barani Ulaya mara tano.

Aidha, Milan haijawahi kushinda mechi za Seria A tangu mwaka 2011 na imemaliza katika nafasi ya 7, 10 na 8 katika misimu mitatu iliyopita.

Kwa sasa inashikilia nafasi ya 6 katika ligi kuu, alama 20 nyuma ya vinara Juventus.
BreakingNews: Kampuni ya China yainunua rasmi klabu ya AC Milani ya Italia BreakingNews: Kampuni ya China yainunua rasmi klabu ya AC Milani ya Italia Reviewed by Zero Degree on 4/13/2017 08:13:00 PM Rating: 5

Powered by Blogger.