Loading...

Mshambuliaji wa zamani wa Chelsea, Didier Drogba ainunua klabu anayoichezea

Maisha ni safari ndefu, baada ya kuzunguka zunguka katika soka hatimaye Didier Drogba amepata klabu mpya, sio tu kama mchezaji mpya bali klabu aliyopata Drogba ni kama mmoja wa wawamiliki wa klabu hiyo.

Klabu hiyo ya Phoenix Rising Fc inayoshiriki ligi imemsajili Didier Drogba, taarifa ya klabu hiyo na Drogba mwenyewe vimeeleza kwamba Drogba ametua katika timu hiyo kama sehemu ya wamiliki wa timu hiyo.

Drogba amesema ushauri kuhusu ununuzi wa timu hiyo ni kutokana na ushauri ambao amekuwa akipewa na mmiliki wa klabu ya Chelsea Roman Abromovich ambaye ni rafiki yake mkubwa.



“Nimekuwa naongea nae(Roman) mara nyingi na kuwa mmiliki wa timu sio kitu rahisi kwa kweli lakini amekuwa akinipa moyo na sasa nimefanikiwa, sio jambo la ajabu ila linaonekana la ajabu kutokana na mambo rafiki zangu wengine wanayofanya” alisema Drogba.

Winga wa zamani wa Chelsea Shaun Wright Philips
Sio Drogba pekeyake kutoka Chelsea ndio aliyeko kwenye timu hiyo lakini pia winga wa zamani wa Chelsea Shaun Wright Philips anacheza katika timu hiyo inayomilikiwa na Didier Drogba.

Drogba anasema Phoeneix Fc ndio sababu ya yeye kuzikataa ofa za kutoka China na Ufaransa ili afanye hicho anachokifanya sasa, pia Drogba amejinasibu kwa kusema hakuna mchezaji mwingine aliyefanya kitu kama hicho lakini hiyo inaonesha jinsi soka lilivyobadilika.

Kati ya maswali ambayo watu wamejiuliza kuhusu umiliki na uchezaji wa Drogba katika klabu hiyo, watu wanawaza itakuwaje endapo kocha hataridhishwa na kiwango chake na kuamua kutompa nafasi?

Drogba anasema “Suala hilo nimekuwa nikiulizwa sana, maamuzi ya kocha yatakuwa ya mwisho na mimi siwezi ingilia maamuzi yake kwa kuwa mimi ni mchezaji tu na nina heshima katika hilo, mimi niko kibiashara hayo mambo ya ufundi uwanjani mimi sijui japo nikicheza soka hadi nikifikisha miaka 40 nitafurahi”
Mshambuliaji wa zamani wa Chelsea, Didier Drogba ainunua klabu anayoichezea Mshambuliaji wa zamani wa Chelsea, Didier Drogba ainunua klabu anayoichezea Reviewed by Zero Degree on 4/13/2017 07:58:00 PM Rating: 5

Powered by Blogger.