Loading...

Pointi tatu ni haki yetu, Kaburu

KLABU ya Simba imewataka wanachama na mashabiki wa timu hiyo kuwa watulivu kusubiri hukumu kuhusiana na malalamiko waliyowasilisha katika Kamati ya Saa 72 ya Uendeshaji na Usimamizi wa Ligi Tanzania.

Simba imewasilisha rufani katika Bodi ya Ligi Kuu kudai pointi za mchezo dhidi ya Kagera Sugar baada ya wenyeji hao kumchezesha kiungo Mohammed Fakhi kwenye mchezo uliofanyika Jumapili iliyopita mjini Bukoba na wenyeji kushinda mabao 2-1.

Makamu wa Rais wa Simba, Geofrey Nyange 'Kaburu' alisema kuwa wanaamini haki itatendeka juu ya malalamiko yao kwa kuzingatia kanuni za kusimamia ligi hiyo zilizowekwa.

"Kamati inafanya kazi kwa kufuata taarifa na si vinginevyo. Taarifa zilizopo bodi ya ligi zipo sahihi na hakuna taarifa zinazogongana. Ukweli ni kweli. Hakuna chembe ya figisu katika suala hili. Kagera walipitiwa katika hili, kanuni zitawaadhibu," alisema Kaburu.

Aliongeza kuwa klabu hiyo inaendelea kuiandaa timu kwa ajili ya mchezo wake dhidi ya Mbao FC utakaofanyika Jumatatu.

'Timu iko Mwanza na vijana wanaendelea na mazoezi kama kawaida, tunaamini nafasi ya kuusaka ubingwa bado tunayo, tutapambana mpaka mechi ya mwisho," alisema kiongozi huyo.

Baada ya kuivaa Mbao FC keshokutwa, Simba itaendelea kubaki Mwanza kuwasubiri Toto Africans katika mechi nyingine ya Ligi Kuu Tanzania Bara itakayofanyika Jumamosi kwenye Uwanja wa CCM, Kirumba.
Pointi tatu ni haki yetu, Kaburu Pointi tatu ni haki yetu, Kaburu Reviewed by Zero Degree on 4/09/2017 02:04:00 PM Rating: 5

Powered by Blogger.