Loading...

Polisi yawatia mbaroni watu 5 waliovamia mkutano wa CUF

JESHI la Polisi Kanda Maalum ya Dar es Salaam kupitia kwa Kamishna, Simon Sirro limesema kuwa limewakamata watuhumiwa watano wanaotuhumiwa kufanya fujo na kusababisha baadhi ya watu katika Mkutano huo waliojeruhiwa kutokana na wavamizi hao kuwa silaha za bastola na mapanga.

Kamishna, Simon Sirro
Kamishna Sirro amesema hayo leo Jumatatu wakati akizungumza na wandishi a habari katika Vinna Hotel Mabibo, amesema jeshi lake lilipokea taarifa ya kuvamiwa kwa Mkutano wa wanachama wa CUF ambapo baada ya taarifa hizo jeshi lake lilifanikiwa kuwakamata jumla ya watuhumiwa watano wanaodaiwa kushiriki katika tukio hilo na akaeleza kuwa watuhumiwa hao wanaendelea kuhojiwa na pindi upelelezi utakapokamilika hatua kali za kisheria zitachukuliwa dhidi yao.

Vilevile ameeleza juu ya baadhi ya watu wanatumia vibaya jina lake hasa nyakati za usiku kwa madai ya kuwa amewaatuma yeye kwa masuala ya migogoro ya kisiasa.

Aidha amefafanua kuwa masuala ya kisiasa siyo jukumu lake kimsingi yeye ni mtumishi wa serikali anayehusika na masuala ya ulinzi na uslama wa raia si vinginevyo, hivyo akawataka wanaofanya hivyo waache tabia hiyo mara moja.
Polisi yawatia mbaroni watu 5 waliovamia mkutano wa CUF Polisi yawatia mbaroni watu 5 waliovamia mkutano wa CUF Reviewed by Zero Degree on 4/24/2017 05:49:00 PM Rating: 5

Powered by Blogger.