Loading...

Rais Magufuli afanya uteuzi mwingine

Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mhe. Dkt. John Pombe Magufuli amemteua Prof. Raphael Tihelwa Chibunda kuwa Makamu Mkuu wa Chuo Kikuu cha Sokoine cha Kilimo (SUA).

Taarifa iliyotolewa na Katibu Mkuu Kiongozi Balozi John Kijazi, Ikulu Jijini Dar es Salaam imeeleza kuwa Uteuzi wa Prof. Raphael Tihelwa Chibunda unaanza leo tarehe 24 Aprili, 2017.

Kabla ya uteuzi huo Prof. Raphael Tihelwa Chibunda alikuwa Mkurugenzi Msaidizi, Idara ya Sayansi na Teknolojia katika Wizara ya Elimu, Sayansi, Teknolojia.

Prof. Raphael Tihelwa Chibunda anachukua nafasi ya Prof. Gerald Monela ambaye amemaliza muda wake.

Wakati huo huo, Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mhe. Dkt. John Pombe Magufuli amewasili Mjini Dodoma ambako pamoja na mambo mengine atakuwa mgeni rasmi katika Sherehe za maadhimisho ya miaka 53 ya Muungano wa Tanganyika na Zanzibar.

Katika uwanja wa ndege wa Dodoma, Mhe. Rais Magufuli amepokelewa na Waziri Mkuu Mhe. Kassim Majaliwa Majaliwa, Spika wa Bunge la Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mhe. Job Ndugai, Waziri wa Nchi Ofisi ya Rais Sera, Bunge, Kazi, Ajira na Walemavu Mhe. Jenister Mhagama na Mkuu wa Mkoa wa Dodoma Mhe. Jordan Rugimbana

Sherehe za Muungano mwaka huu, zitafanyika katika Uwanja wa Jamhuri ikiwa ni mara ya kwanza kufanyika katika makao makuu ya nchi Mjini Dodoma.

Na Gerson Msigwa Mkurugenzi wa Mawasiliano ya Rais, IKULU Dar es Salaam
Rais Magufuli afanya uteuzi mwingine Rais Magufuli afanya uteuzi mwingine Reviewed by Zero Degree on 4/25/2017 02:39:00 AM Rating: 5

Powered by Blogger.