Loading...

Rais Magufuli alaani mauaji ya askari yaliyotokea Pwani, ....atuma salamu za pole kufuatia tukio hilo

Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mhe. Dkt. John Pombe Magufuli amepokea kwa mshtuko na masikitiko makubwa taarifa za vifo vya Askari Polisi 8 waliouawa kwa kushambuliwa na watu wenye silaha jana jioni tarehe 13 Aprili,2017 katika eneo la Jaribu Mpakani,Wilayaya Kibiti Mkoani Pwani.

Askari Polisi hao walikuwa wakitoka kubadilishana doria na wameshambuliwa kwa kupigwa risasi wakiwa wanasafiri kwa gari katika barabara ya Dar es Salaam – Lindi.

Mhe. Rais Magufuli amemtumia salamu za rambirambi Mkuu wa Jeshi la Polisi nchini IGP-Ernest Mangu,familia za askari wote waliouawa, Askari Polisi wote na Watanzania wote walioguswa na vifo hivyo.

“Nimeshtushwa na nimesikitishwa sana na vifo vya askari wetu 8 ambao wamepoteza maisha wakiwa wanalitumikia Taifa,naungana na familia za marehemu wote, Jeshi la Polisi na Watanzania wote katika kipindi hiki kigumu cha huzuni na majonzi ya kuondokewa na vijana wetu shupavu.

“Namuomba Mwenyezi Mungu atupe moyo wasubira, uvumilivu na ustahimilivu”amesema Mhe.Rais Magufuli.

Aidha, Mhe. Dkt. Magufuli amelaani tukio hilo na matukio yote yakuwashambulia askari polisi ambao wanafanyakazi kubwa na muhimu ya kulinda raia na mali na ametakaWatanzania wote watoe ushirikiano katika kukomesha vitendo hivyo.

Mhe. Rais Magufuli amewaombea marehemu wote wapumzishwe mahali pema peponi, Amina.
Rais Magufuli alaani mauaji ya askari yaliyotokea Pwani, ....atuma salamu za pole kufuatia tukio hilo Rais Magufuli alaani mauaji ya askari yaliyotokea Pwani, ....atuma salamu za pole kufuatia tukio hilo Reviewed by Zero Degree on 4/14/2017 12:52:00 PM Rating: 5

Powered by Blogger.