Loading...

BreakingNews: Majambazi yauwa askari polisi 7 mkoani Pwani na kutokomea kusikojulikana

Polisi saba waliokuwa doria katika Kijiji cha Jaribu mpakani mwa wilaya za Rufiji na Kibiti mkoani Pwani, wanadaiwa kuuawa usiku huu kwa kupigwa risasi na watu wasiofahamika.

Mkuu wa Jeshi la Polisi, IGP Ernest Mangu
Mkuu wa Jeshi la Polisi, IGP Ernest Mangu amethibitisha kutokea kwa mauaji hayo, lakini akasema taarifa zaidi zitatolewa na kamanda wa polisi wa Mkoa wa Pwani.

Taarifa za uhakika zilizolifikia Mwananchi Digital zimeeleza kuwa polisi hao walikuwa kwenye gari wakirejea kituoni kutoka doria na walishambuliwa na watu waliotokea msituni.

Taarifa zaidi fuatilia ukurasa huu>>>
BreakingNews: Majambazi yauwa askari polisi 7 mkoani Pwani na kutokomea kusikojulikana BreakingNews: Majambazi yauwa askari polisi 7 mkoani Pwani na kutokomea kusikojulikana Reviewed by Zero Degree on 4/14/2017 12:24:00 AM Rating: 5

Powered by Blogger.