Loading...

Disko toto marufuku mkoani Shinyanga

Picha ya Mtandao
Jeshi la polisi mkoani Shinyanga limepiga marufuku madisko ya watoto maarufu kama ‘disko toto’ katika vipindi vyote vya sikukuu huku likiwataka wakazi wa mkoa wa Shinyanga kusherehekea sikukuu ya pasaka kwa amani na upendo na kuepuka vitendo vinavyoweza kusababisha vurugu kwa kukiuka sheria za nchi.

Akitoa kauli hiyo mbele ya waandishi wa habari Kamanda wa Jeshi la polisi mkoa wa Shinyanga ACP muliro Jumanne Muliro amesema vikosi vya polisi mkoani humo vimejiandaa kukabiliana na vitendo vya uhalifu vinavyoweza kujitokeza wakati wa sikukuu ya pasaka huku akiwataka wakazi mkoani hapa kuchukua tahadhari kwa kuacha angalau baadhi ya watu majumbani mwao kwa ajili ya kulinda usalama.

Katika hatua nyingine Kamanda Mulito ametoa taarifa juu ya msako na ukamataji wa pombe aina ya viroba uliyoanza mwanzoni mwa mwezi wa tatu na kudai kuwa hadi kufikia tarehe ya leo jumla ya katoni 13,859 zenye thamani ya shilingi 946,114,800 zimekamatwa na msako bado unaendelea.

Akikamilisha taarifa hiyo Kamanda Muliro amesema lengo sio kuwatisha wananchi bali ni kuhakikisha wananchi wanakua salama katika maeneo yao na mkoa kwa ujumla.
Disko toto marufuku mkoani Shinyanga Disko toto marufuku mkoani Shinyanga Reviewed by Zero Degree on 4/14/2017 12:29:00 AM Rating: 5

Powered by Blogger.