Loading...

Rais Magufuli awasili Pugu kuweka jiwe la msingi ujenzi wa Reli ya kisasa

Rais John Magufuli ameshafika katika eneo la Pugu nje kidogo ya jiji la Dar es Salaam kwa ajili ya kuweka jiwe la msingi la ujenzi wa reli mpya ya kisasa ya Standard Gauge itakayotumia umeme.

Ujenzi huo unaashiria kuingia hatua ya pili ya ujenzi baada ya ile ya awali ambapo mkataba wa. ujenzi ulitiwa saini na kampuni hodhi ya rasilimali za reli nchin Rahco na kampuni wabia wa zabuni ambao ni kampuni ya Merkez ya Uturuk na Mota-Engil ya Ureno Februari 3 mwaka huu.

Gharama za ujenzi huu awamu ya kwanza kati ya DSM mpaka Morogoro itagharimu shilingi Trilion 2.7.

Aidha, mradi huo utakapokamilika utarahisisha usafiri wa kutoka Dar es salaam hadi katika mikoa ya Morogoro, Dodoma na Mwanza.

Kwa upande wake Mkurugenzi Mkuu wa Kampuni ya Reli (RAHCO), Masanja Kadogosa alisema kuwa kukamilika kwa ujenzi huo kutarahisisha shughuli za usafiri na usafirishaji kwa kuwa safari ya Dar es salaam hadi Morogoro itatumia muda wa saa 1:16, huku Dar es salaam hadi Dodoma itatumia masaa 2:30 na safari ya Dar es salaam hadi Mwanza itatumia masaa 7:30.

Mradi huo ambao uko chini ya Kampuni za Merkezi ya Uturuki na Mota-Engil Afrika ya Ureno, kwa awamu ya kwanza utaanza na kipande cha kilomita 300 kati ya Dar es salaam hadi Morogoro kwa gharama za dola bilioni moja za Marekani.
Rais Magufuli awasili Pugu kuweka jiwe la msingi ujenzi wa Reli ya kisasa Rais Magufuli awasili Pugu kuweka jiwe la msingi ujenzi wa Reli ya kisasa Reviewed by Zero Degree on 4/12/2017 10:31:00 AM Rating: 5

Powered by Blogger.