Ekari zaidi ya 50 za bangi zilizokuwa zikilimwa kwa umwagiliaji zateketezwa mkoani Njombe.
Serikali mkoani Njombe imebaini uwepo wa mashamba makubwa ya bangi katika wilaya ya Makete kijiji cha Ngonde ambapo katika hali ya kushangaza wakulima wanatumia pembejeo za kilimo na teknolojia ya umwagiliaji Kuzalisha bangi katika mabonde kwa kuchanganya na mazao mengine yakiwemo mahindi.
Mkuu wa mkoa wa Njombe akiwa na kamati ya ulinzi na usalama ya mkoa amefanya ziara katika kijiji hicho pamoja na kushiriki uteketezaji wa bangi kwa zaidi ya ekari 50 lakini pia ametoa maagizo kwa viongozi wa wilaya vijiji na vitongoji.
Ni zaidi ya siku tatu kamati ya ulinzi imetumia kusaka na kuteketeza bhangi ambapo hata hivyo ni mtu mmoja tu aliyekamatwa huku wengine wakiendelea kusakwa ili wafikishwe kwenye vyombo vya sheria.
Baadhi ya wananchi wilayani Makete wamesema kuwa zao hilo wamekuwa wakilitumia tangu kale kama kiungo cha mboga lakini sasa matumizi yamebadilika na kuwa madawa ya kulevya hivyo jamii inatakiwa kuacha kuendelea kuzalisha zao hilo.

Source: ITV
Ekari zaidi ya 50 za bangi zilizokuwa zikilimwa kwa umwagiliaji zateketezwa mkoani Njombe.
Reviewed by Zero Degree
on
4/12/2017 10:37:00 AM
Rating: