Loading...

Rwakatare ateuliwa kuwa Mbunge viti maalum kujaza pengo la Sophia Simba

Mchungaji Getrude Rwakatare 
Mchungaji wa Kanisa la Assemblies Of God Mikocheni B jijini Dar es Salaam, Dk Getrude Rwakatare amechaguliwa kuwa Mbunge wa Viti Maalum kujaza iliyoachwa wazi na Sophia Simba.

Mkurugenzi wa Tume ya Uchaguzi (NEC) Ramadhan Kailima akizungumzia uteuzi huo alisema CCM ilipeleka jina la Mchungaji Rwakatare ambapo walipitia fomu zake na kuridhika kuwa ana sifa za kuwa mbunge.

Sophia Simba ambaye alikuwa mwenyekiti wa Umoja wa Wanawake wa CCM (UWT) alifukuzwa uanachama wa chama hicho kwa madai ya ukiukwaji wa maadili ya chama Machi 11, mwaka huu hali iliyomfanya kukosa sifa ya kuendelea kuwa mbunge kwa mujibu wa Katiba ya nchi.

Rwakatare ateuliwa kuwa Mbunge viti maalum kujaza pengo la Sophia Simba Rwakatare ateuliwa kuwa Mbunge viti maalum kujaza pengo la Sophia Simba Reviewed by Zero Degree on 4/15/2017 09:05:00 AM Rating: 5

Powered by Blogger.