Loading...

Huu ndio uamuzi uliouchukuliwa na uongozi wa Kagera Sugar baada ya kupokonywa pointi 3 na kamati ya saa 72

Siku moja baada ya Kamati ya saa 72 kupitia Mwenyekiti wake Hamadi Yahaya kutangaza kuwa Simba imeshinda rufaa yake dhidi ya Kagera Sugar ambayo ilimchezesha Mohamed Fakhi akiwa na kadi tatu za njano, Kagera Sugar wameandika barua ya kuomba shauri lao lisikilizwe tena.

Kagera Sugar imefikia maamuzi hayo baada ya kujiridhisha kuwa mchezaji wao Mohamed Fakhi hana kadi tatu za njano kama ambavyo wameadhibiwa na kupokonywa point na bodi ya Ligi, hivyo wanaomba lipitiwe upya shauri lao na kuhakikisha haki inatendeka.

Kama utakuwa unakumbuka Simba na Kagera Sugar zilicheza April 2 2017 katika uwanja wa Kaitaba Bukoba na Simba ikapoteza kwa kufungwa magoli 2-1, ila baada ya hapo walikata rufaa kwa kuituhumu Kagera Sugar kumchezesha mchezaji Mohamed Fakhi akiwa na kadi tatu kinyume na taratibu.


Huu ndio uamuzi uliouchukuliwa na uongozi wa Kagera Sugar baada ya kupokonywa pointi 3 na kamati ya saa 72 Huu ndio uamuzi uliouchukuliwa na uongozi wa Kagera Sugar baada ya kupokonywa pointi 3 na kamati ya saa 72 Reviewed by Zero Degree on 4/15/2017 09:17:00 AM Rating: 5

Powered by Blogger.