Loading...

Salma Kikwete aapishwa leo, ...hili ndilo swali lake la kwanza Bungeni mara baada ya kula kiapo

Mama Salma akiingia Bungeni.
Spika wa Bunge la Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Job Ndugai, leo amemwapisha kuwa Mbunge wa Kuteuliwa, Mh. Salma Kikwete, ambaye ni mke wa rais mstaafu wa awamu ya nne, Jakaya Kikwete.

Mbunge huyo aliandamana na mumewe ambaye alisababisha kelele za shamra kutoka kwa wabunge waliokuwa wakisema: “Tumekumiss…Tumekumiss…”

Salma Rashid Kikwete amekula kiapo leo asubuhi katika mkutano wa saba wa Bunge la bajeti na kuwa mbunge halali wa Bunge la Jamhuri ya Muungano wa Tanzania.

Kwa mijibu wa taarifa iliyotolewa na Kurugenzi ya Mawasiliano ya Rais, Ikulu Machi 1 mwaka huu, ilieleza kuwa, Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Dkt. John Pombe Magufuli, amemteua mama Salma Kikwete kuwa Mbunge wa bunge la Jamhuri ya Muungano wa Tanzania.

Salma Kikwete ameapishwa leo kabla ya shughuli za Bunge kuendelea ambapo miongoni mwa waliohudhuria tukio hilo la kuwapishwa ni mumewe, Rais Mstaafu Dkt Jakaya Mrisho Kikwete.

Baada ya kuapa, Salma Kikwete amepata nafasi ya kuuliza swali lake la kwanza kama mbunge na alilielekeza kwa Waziri wa Nchi, Ofisi ya Rais Menejimenti ya Utumishi wa Umma na Utawala Bora ambapo alitaka kujua, ni upi mpango madhubuti wa serikali katika kutumia fedha za TASAF kusaidia watu maskini mkoani Lindi?

Aidha, Waziri Kairuki alijibu kuwa serikali imejipanga kuhakikisha kuwa inatumia fedha hizo kusaidia kutokomeza umasikini nchini kote kwani inatambua kuwa, umasikini ni kikwazo kikubwa katika kujikwamua kiuchumi.

Rais mstaafu wa awamu ya nne, Jakaya Kikwete (katikati) akiwa Bungeni.
Ujumbe wa Rais Mstaafu J. Kikwete mtandaoni.
Salma Kikwete aapishwa leo, ...hili ndilo swali lake la kwanza Bungeni mara baada ya kula kiapo Salma Kikwete aapishwa leo, ...hili ndilo swali lake la kwanza Bungeni mara baada ya kula kiapo Reviewed by Zero Degree on 4/04/2017 11:04:00 AM Rating: 5

Powered by Blogger.