Wanaume waliokuwa wamevaa hijabu wauawa kwa kupigwa risasi na polisi mkoani Pwani
Kamanda wa Polisi mkoani Pwani, Onesmo Lyanga |
Akizungumza na waandishi wa habari ofisini kwake mjini Kibaha, Kamanda wa Polisi mkoani Pwani, Onesmo Lyanga, alisema pikipiki nyingine mbili zilifanikiwa kukimbia.
Lyanga akielezea juu ya tukio hilo, alisema limetokea Aprili 2, mwaka huu saa 6:00 mchana Mwembe Muhoro Wilaya ya Rufiji.
“Siku ya tukio askari walipata taarifa kuwa kulikuwa na pikipiki tatu zikitokea Kibiti kwenda mikoa ya Kusini zikiwa zimebeba watu watatu kila moja huku miongoni mwa pikipiki hizo kati yake mbili wamebebwa watu waliovaa hijabu,” alisema Kamanda Lyanga.
Alisema askari wa barabarani walipewa taarifa katika kizuizi cha Mparange na kuwasimamisha ili wawahoji, lakini walikataa na kupita ambapo waliwajulisha wenzao kwenye kizuizi cha Ikwiriri, lakini walikaidi kusimama kupita kwa kasi.
“Baada ya hapo walifika katika kizuizi cha Ikwiriri, lakini bado walikaidi kusimama na kuendelea kukimbia ndipo walipofika kituo cha Mwembe Muhoro hata hivyo hawakusimama na askari waliokuwa doria wakiwa kwenye gari waliwafuatilia na wakavuka Daraja la Mkapa na waliwapa onyo kwa kupiga risasi hewani,” alifafanua.
Alisema baada ya hapo watu hao waliruka kwenye pikipiki na kuanza kukimbilia msituni na ndipo askari walipowapiga risasi za miguu na kiunoni na kuwakamata.
“Majeruhi hao walijulikana ni wanaume hata hivyo majina yao hayakuweza kufahamika na walikuwa kwenye pikipiki yenye namba za usajili MC 272 BLW aina ya Boxer yenye rangi nyeusi ambapo watu hao wanaodhaniwa kuwa ni wahalifu kwa mwonekano wao walijaribu kuwawahisha Hospitali ya Misheni ya Mchukwi,” alieleza kamanda.
Alisema walipofikishwa hospitali daktari alithibitisha kuwa watu hao wamekufa ambapo hata hivyo majina yao hayakuweza kufahamika huku pikipiki nyingine mbili zilitoroka na kuelekea Mkoa wa Lindi na taarifa zimetolewa polisi ili wawakamate.
Aliwataka wananchi kuwa watulivu wanaposimamishwa na askari polisi badala ya kujaribu kutoroka na kwa sasa jeshi hilo limeimarisha doria katika kukabiliana na uhalifu.

Reviewed by Zero Degree
on
4/04/2017 11:43:00 AM
Rating: