Serikali yataifisha Majahazi 8 mkoani Tanga kwa kuingiza bidhaa za magendo kwenye bandari bubu.
Serikali mkoani tanga imetaifisha majahazi nane yenye thamani ya zaidi ya shilingi milioni 100 kisha wamiliki wake kutozwa faini baada ya vyombo vyao kukutwa kwa nyakati tofauti vikiwa vimeingiza bidhaa mbali mbali nchini zenye thamani ya mamilioni ya shilingi kupitia bandari bubu bila kulipiwa ushuru.
Hatua hiyo ni jitihada zilizofanywa na watendaji wa mamlka ya mapato nchini (tra) tawi la tanga kwa kushirikiana na jeshi la polisi kwa kukamata bidhaa mbali mbali ikiwemo sukari, mafuta ya kupikia, dawa, vipuri vya magari pamoja na majola ya mashuka yaliyokamatwa kwa nyakati tofauti katika operesheni ya pamoja ya kudhibiti ukwepaji kodi.
Kufuatia hatua hiyo, bwana magoti amewataka wafnyabiahsra hasa wa kutoka kisiwani zanzibar kuheshimu sheria za nchi kwa kuingiza bidhaa zao kihalali na kulipa kodi kwa serikali kwa sababu hatua hiyo itasababisha baadhi yao wenye mitaji midogo kufunga biashara zao kwa sababu ya kukwepa ushuru.
Kufuatia hatua hiyo, bwana magoti amewataka wafnyabiahsra hasa wa kutoka kisiwani zanzibar kuheshimu sheria za nchi kwa kuingiza bidhaa zao kihalali na kulipa kodi kwa serikali kwa sababu hatua hiyo itasababisha baadhi yao wenye mitaji midogo kufunga biashara zao kwa sababu ya kukwepa ushuru.
Serikali yataifisha Majahazi 8 mkoani Tanga kwa kuingiza bidhaa za magendo kwenye bandari bubu.
Reviewed by Zero Degree
on
4/01/2017 12:54:00 PM
Rating: